sport news

Goal inakuchambulia tathimini ya ligi kuu bara kwa msimu

Timu mbali mbali zipo kwenye maandalizi kwa ajili ya msimu mpya unao tarajiwa kuanza mwishoni mwa mwezi wa 8, msimu mpya unatarajiwa kuwa na ushindani mkumbwa hasa kutokana na vilabu mbali mbali kufanya maboresho kwenye mabenchi ya ufundi na wachezaji. Wanachama na viongozi wa Simba wanataka kuiona timu yao ikuchukua ubingwa huku wapinzani wao Yanga nao wanaitaji kulitetea taji lao, Azam pia chini ya Muhispania nao wanataka kitu msimu ujao, vita ya kushuka daraja nayo ni mgumu kwa msimu ujao.

Mbio za ubingwa


Licha ya Simba kupania kufanya vizuri msimu ujao, ila nafasi ya ubingwa kwa msimu 2016/2017 ni Yanga na Azam, hasa kutokana na ubora wa vikosi vyao, wachezaji wamekaa pamoja zaidi ya misimu 3 tofauti ya Simba ambayo itaanza msimu ikiwa na ingizo jipya la wachezaji zaidi ya 13 na benchi la ufundi jipya hivyo wanaitaji muda wachezaji na benchi la ufundi kuelewana taratibu.

Nafasi nne za juu


Bila shaka msimu msimu ujao nafasi 3 za juu bado Simba, Yanga na Azam wataendelea kuzitawala, ila vita hipo kwenye nafasi ya 4, timu zenye nafasi kubwa ya kukamata nafasi ya 4 ni Mtibwa na Mwadui hasa kutokana na ubora wa makocha wao wenye uzoefu na ligi kuu bara, timu kama Kagera Sugar na Mbeya City licha ya kufanya vibaya msimu uliopita, msimu mpya wataibuka na kufanya vizuri sababu kuu ni maboresho waliyo yafanya kuanzia kwenye benchi la ufundi hadi wachezaji.

Ufungaji bora


Kumekuwa na changamoto kubwa sana hasa kwa washambuliaji wazawa kwa kutofanya vizuri kwenye kufamania nyavu, bado nafasi ya ufungaji bora msimu ujao inatazamiwa kwenda kwa mgeni kama msimu ulio malizika, wazawa wamekuwa hawana mwendelezo wa kufanya vizuri kwenye ligi kuu viwango vyao vimekuwa vikipanda na kushuka.

Timu za kushuka daraja


Kumekuwa na utaratibu wa timu zilizo panda ligi kuu kushuka tena baada ya msimu mmoja timu kama Mbao fc, Majimaji, Toto, African lyon, Ruvu Shooting zina pewa nafasi kubwa ya kushuka daraja hasa kutokana na maandalizi hafifu na kutokuwa na wafadhili kwa baadhi ya timu, pia timu kama Stand United inapigiwa kura nyingi ya kushuka daraja sababu ya mgogoro unao endelea ndani ya klabu na kuitelekeza timu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *