news

Mwanamke mhanga alipua msikiti wa Maiduguri, Nigeria

Watu nane wamefariki baada ya mwanamke kujilipuwa msIkitini, Kaskazini Mashariki mwa Nigeria.

Watu hao wameuawa jana , Jumatatu kufuatilia mwanamke mmoja kudaiwa kujilipua kwa bomu katika msikiti nchini humo.

Mkuu wa shirika la usimamizi wa dharura, Ahmed Satomi, alisema mlipuko huo umejeruhi watu wengine kumi na tano, London Ciki Maiduguri.

Msikiti ulikuwa unalindwa na raia wa JTF wakati wa sala, aliwaambia AFP

Kulikuwa na wasichana wawili ambao walitaka kushambulia msikiti, ambaye mmoja alinaswa kwenye uzio wenye umeme mwingine alifanikiwa kukimbia huku akikimbizwa na polisi, alisema Danbatta Bello.

Alikimbilia msikitini na walinzi walimuamuru asimame ili wamkague lakini ghafla mwanamke huyo alikimbilia ndani ya msikiti na kutegesha bomu lake la pili.

Msikiti ulianguka baada ya bomu kulipuka na hadi sasa polisi hajasema chochote kuhusiana na mlipuko huo.

Wanawake wengine wawili nao waliouawa kwa kupigwa risasi baada ya kushukiwa kuwa ni miongoni mwa kundi hilo la kujitoa mhanga huko Maiduguri baada ya mlipuko wa msikitini, alisema Bello.

Boko Haram wanasadikiwa kuhusika na tukio hilo na pia inasemekana kuwa kundi hilo linawatumia wanawake na wasichana wadogo kufanya mashambulizi mbalimbali.

Hivi karibuni mabinti waliofanikiwa kutoroka kutoka kwa kundi hilo walisema wasichana hao waliokamatwa na Boko Haramu hupewa dawa za Kulevya na kulazimishwa kufanya matukio ya kujitoa muhanga.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *