sport news

Majimaji yazifuata point 3 za Iringa

Kikosi cha Majimaji wanalizombe kimeondoka mjini Songea mapema leo kuifuata Lipuli FC ya Iringa tayari kwaajili ya mchezo wao wa ligi kuu Tanzania Bara utakaopigwa kesho katika dimba la Samora.

Wanalizombe hawajapata ushindi wowote tangu kuanza kwa ligi wakisalia katika nafasi ya tatu kutoka mkiani mwa ligi tofauti na wenzao wa Lipuli ambao wanajivunia ushindi katika mchezo mmoja.

Msemaji wa Majimaji Onesmo Ndunguru amesema wanakwenda Iringa kuchukua point 3 ili kujiondoa katika nafasi waliyopo sasa, kwani wamechoka kupata matokeo ya kupoteza na kupat sare.

Amesema kikosi kiko katika hali nzuri na mwalimu ameshafanyia marekebisho makossa yaliyojitokeza katika mchezo uliopita dhidi ya Ndanda FC uliomalizika kwa sare ya bao 1-1.

Mcheo huu utakufikia moja kwa moja kupitia channel ya ZBC 2 inayopatikana ndani ya kingamuzi cha Azam TV.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *