sport news

Julio aipa ubingwa Azam FC

Kocha wa Dodoma FC inayoshiriki ligi daraja la kwanza, Jamhuri Kihwelo Julio ameitabiria ubingwa wa ligi kuu Tanzania Bara timu ya Azam FC msimu huu.

Julio ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na afisa habari wa Azam FC, Jaffary Idd wakati timu zao zilipokuwa zikifanya mazoezi ya pamoja katika Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.

Kihwelo amesema kwa mtazamo wake katika timu zote 16 zinazoshiriki ligi kuu msimu huu, ni Azam pekee ambayo imejiwekea mipango inayoeleweka na inateikeleza ikiwemo kutilia mkazo soka la vijana.

Pia amesema hadi sasa akiangalia mwenendo wa klabu hiyo kwenye ligi, anaona kuna kila dalili za mafanikio makubwa mbeleni.

Azam FC imeweka mapumziko ya muda mfupi mjini Dodoma wakati ikielekea Shinyanga kwa ajili ya mchezo wa ligi kuu dhidi ya Mwadui FC Jumamosi hii utakaorushwa mbashara na Azam TV.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *