news

UBUNGE WA SALMA KIKWETE GUMZO

SIKU moja baada ya Rais Dk. John Magufuli kumteua mke wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Salma Kikwete kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mjadala mkali umeibuka kutokana na uteuzi wake. Watu wa kada mbalimbali wakiwemo wasomi na wachambuzi wa masuala ya kisiasa, wameuchambua uteuzi huo kwa kuupinga na wengine kuupongeza. Salma ambaye ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, akitokea Wilaya ya Lindi Mjini, amekuwa akitajwa kujitosa katika kinyanganyiro cha ubunge Jimbo la Lindi Mjini, katika uchaguzi ujao. Baadhi ya wachambuzi wanautazama uteuzi huo kama ni hatua ya kuimarisha uhusiano kati ya utawala wa Rais Mstaafu Jakaya Kikwete na utawala wake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *