news

Trump ampigia simu Xi Jinping na kukubali msimamo kuhusu China
Rais wa Marekani Donald Trump amekubali kuheshimu kile anachokiita sera ya "China Moja" pale alipompigia simu Rais wa China Xi Jinping, Ikulu ya White House imesema.
Sera ya China Moja ni elimu ya kidiplomasia, kwamba kuna serikali moja tu iitwayo China.
Bwana Trump alitilia shaka sera ya muda mrefu ya china, pale alipofanya mazungumzo na Rais wa Taiwan ,mwezi Desemba.
Hiyo ni mojawepo ya hatua kubwa mno ya kuvunja tamaduni ya muda mrefu ya kufuata taratibu ya uongozi, na kuchochea malalamiko rasmi kutoka kwa utawala wa China.
Mazungumzo hayo ya simu ni ya kwanza kati ya marais hao wawili tangu Trump alipoingia ofisini Januari 20, licha ya Rais Trump kuwapigia simu viongozi wa mataifa kadhaa duniani.