news

Tetemeko la ardhi latikisa Zambia na Tanzania

Tetemeko la ardhi ya ukubwa wa 5.7 kwenye vipimo vya Richter limekumba maeneo ya Ziwa Tanganyika usiku wa kuamkia leo.

Tetemeko hilo lilitikisa maeneo ya kaskazini mwa Zambia na mitetemeko hiyo ikasikika maeneo ya kusini magharibi mwa Tanzania, hasa eneo la Rukwa. Kitovu cha tetemeko hilo, kwa mujibu wa Shirika la Utafiti wa Jiolojia la Marekani, kilikuwa kilomita 10 chini ya ardhi umbali wa kilomita 45 mashariki mwa mji wa Kaputa nchini Zambia.

Mji huo unapatikana katika mpaka wa nchi hiyo na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Tetemeko hilo lilitokea mwendo wa saa tisa na dakika thelathini na mbili usiku (0032 GMT). Waathiriwa wa tetemeko Bukoba, Tanzania waomba msaada Magufuli: Serikali haikusababisha tetemeko Kagera

Tetemeko la ardhi la ukubwa kama huo huchukuliwa kuwa la kadiri lakini wataalamu wanasema kutokana na hali kwamba kitovu chake chakikuwa chini sana ndani ya ardhi, huenda hilo lilisababisha mitikisiko kuwa mikubwa.

Desemba mwaka 2005, tetemeko kubwa la ardhi lilitokea eneo la Ziwa Tanganyika. Tetemeko hilo la nguvu ya 6.8 lilitikisa majumba katika miji maeneo ya Afrika mashariki na kati.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *