sport news

Real Madrid wachapwa mechi ya pili mfululizo

Real Madrid wameshindwa kwenye mechi ya pili mfululizo kwa mara ya kwanza tangu Novemba 2015 baada ya Celta Vigo kuwalaza 2-1 mechi ya mkondo wa kwanza robofainali ya Kombe la Mfalme, Copa del Rey..

Madrid, ambao mkimbio wao wa kutoshindwa mechi 40 ulifikishwa kikomo na Sevilla siku ya Jumapili, walijipata nyuma kwenye mechi pale mshambuliaji wa zamani wa Liverpool Iago Aspas alipofunga bao lake la 16 msimu huu.

Madrid walisawazisha kupitia Marcelo lakini Jonny akawahakikishia ushindi baada ya kufunga sekunde chache baadaye kupitia kaunta kwenye mechi hiyo iliyochezewa Bernabeu.

Real Madrid yaweka rekodi ya mechi 40 bila kushindwa Mfaransa Karim Benzema alipoteza nafasi nzuri kombora lake lilipopaa juu ya goli zikiwa zimesalia dakika nane mechi kumalizika. Mechi ya marudiano itachezewa Galicia Jumatano wiki ijayo.

Real Madrid, chini ya Zinedine Zidane, walikuwa wameshindwa mechi mbili pekee kati ya 48 walizocheza karibuni zaidi mashindano yote.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *