news

Oprah Winfrey kuwania urais Marekani?

Oprah Winfrey huenda akawania urais kufuatia hatua ya rais Donald Trump kushinda urais. Aliambia runinga ya Bloomberg kwamba kuchaguliwa kwa Trump licha ya yeye kukosa uzoefu wowote wa kisiasa kumemfanya kufikiria kuhusu uwezo wake wa afisi hiyo kuu. Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 63 ambaye amekuwa akishiriki katika kipindi cha mazungumzo na ambaye alimuunga mkono Hillary Clinton awali alikuwa akifutilia mbali maswali ya yeye kuingia siasa. Lakini sasa ametoa ishara ya kutaka kua mgombea wa wadhfa huo. ''Sikufikria swala hilo hata kidogo'', aliambia mfadhili David Rubenstein katika kipindi chake katika runinga ya Bloomberg alipoulizwa iwapo atakubali kuwania wadhfa huo.''Nilifikiria,Oh.. Oh''? Akimfananisha na Trump ,bw Rubenstein alisema kuwa sio kwamba mtu anahitaji uzoefu wa kuwa serikalini kuchaguliwa kuwa rais wa Marekani. ''Hivyo ndivyo nilivyofikiri, aliongezea nilidhani sina uzoefu, sina ufahamu mwingi, aliongezea, nilifikiri ..Oh sina uzoefu mwingi na sasa nafikiria Oh''.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *