news

Mihadarati ya Cocaine ya pauni milioni 50, yapatikana Uingereza

Mamlaka kuu ya kukabiliana na uhalifu nchini Uingereza, imesema kuwa dawa ya kulevya aina ya Cocaine, yenye kiasi cha pauni milioni 50, imepatikana ikiwa imesombwa na maji hadi katika ufukwe wa Norfolk, Nchini Uingereza.

Zaidi ya kilo 360 ya mihadarati hiyo ilipatikana imesombwa hadi katika ufukwe wa Hopton, karibu na Great Yarmouth na ufukwe mwingine ulioko hapo karibu wa Caister.

Mwananchi mmoja alifahamisha maafisa wa polisi wa kituo cha Norfolk, baada ya kugundua mabegi yaliyokuwa na dawa hizo za kulevya katika ufukwe wa Hopton.

Polisi na maafisa wa mamlaka hiyo kuu ya kupambana na uhalifu wanaendelea kusaka maeneo hayo.

Matthew Rivers, kutoka mamlaka hiyo kuu (NCA), na askari wa kulinda mipaka ya nchi, anasema kuwa: "tunafanya kazi pamoja na kikosi cha kulinda mpaka, idara ya polisi wa pwani, na maafisa wa polisi wa kituo cha Norfolk, ili kubaini namna mifuko hiyo ilifikishwa hapo, hata hivyo ni jambo la kutamausha ikiwa kweli madawa hayo yallikuwa yakifikishwa Uingereza.

"Bila shaka hii ni shehena kubwa Zaidi ya dawa za kulevya kupatikana, na kupotea kwake ni pigo kubwa kwa magenge ya uhalifu yanayohusika Superintended Dave Buckley, kutoka jimbo la Norfolk Constabulary, anasema: "Huku tukiamini kuwa tumepata shehena yote, raia yeyote akipata dawa zingine, tunaomba atufahamishe mara moja.

"Tunao maafisa wa ziada watakaosalia katika eneo hilo ili kuendesha uchunguzi na kufuatilia taarifa zozote ambazo zinaweza kuchipuka." Dave Buckley alisema

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *