news

Marekani yataka suluhu Israel na Palestina

Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa amesema nchi yake inaunga mkono wazo la suluhu ya mataifa mawili katika mgogoro wa Israel na Palestine. Lakini, Nikki Haley pia amesema utawala wa rais Trump unaangalia uwezekano wa kupatikana kwa suluhu nyengine.

Kwa miaka mingi, Marekani imekuwa ikiunga mkono kuanzishwa kwa taifa la Palestine kando na Israel. UN yamuonya Trump kwa msimamo kuhusu Israel na Palestina

Trump aitaka Israel kusitisha ujenzi katika ardhi ya Palestina Lakini, bwana Trump amesema siku ya Jumatano kwamba hilo hatolisisitizia. Amesema, mwisho wa siku, ni juu ya pande mbili zinazohasimiana kutatua mgogoro huo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *