news

Jammeh akataa kuachia uongozi Gambia

Rais wa Gambia Yahya Jammeh amekataa kuondoka madarakani kutoa nafasi ya kuapishwa kwa Adama Barrow hata baada ya makataa aliyopewa na Senegal kumalizika.

Barrow alipangiwa kuapishwa kuwa rais mpya Alhamisi, na wanajeshi wa nchi za Afrika Magharibi wako tayari kuingilia kati. Rais wa Mauritania Mohamed Ould Abdel Aziz alikutana na Bw Jammeh kwa mazungumzo ya dakika za mwisho kabla ya kuondoka na kwenda Senegal kwa mazungumzo na rais Macky Sall.

Bw Barrow alitangazwa kuwa mshindi wa uchaguzi mkuu mwezi uliopita na Bw Jammeh mwanzoni alikubali kushindwa lakini baadaye akapinga matokeo hayo. Kiongozi wa upinzani ashinda uchaguzi wa urais Gambia

Wasifu wa rais mteule wa Gambia Adama Barrow Wanajeshi wa Senegal wamesalia kwenye mpaka wa nchi hiyo na Gambia, huku muda wa mwisho aliowekewa Bw Jammeh na Senegal kuondoka madarakani - saa sita usiku - ukipita.

Pendekezo la wanajeshi wa mataifa ya Afrika Magharibi kuingilia kati kumuondoa madarakani linaungwa mkono na Nigeria na nchi nyingine za kanda hiyo. Mkuu wa majeshi ya Gambia Ousman Badjie amesema wanajeshi wake hawatapigana na wanajeshi wa Senegal iwapo wanajeshi hao wataingia nchini Gambia, shirika la habari la AFP limeripoti.

"Hatutahusika kijeshi, huu ni mzozo wa kisiasa," amesema. "Sitashirikisha wanajeshi wangu katika mapigano ya kipuuzi. Nawapenda wanajeshi wangu."

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *