news

China yakubali kuirejesha manuwari ya Marekani

Idara ya ulinzi nchini Marekani Pentagon imesema kuwa imeafikiana na China kwamba itairejesha manuwari iliopatikana katika bahari ya kusini mwa China.
.
China iliikamata manuwari hiyo katika maji ya kimataifa siku ya Alhamisi. Haijasema ni kwa nini ilichukua hatua hiyo na kuishutumu Marekani kwa kulifanya jambo hilo kuwa kubwa..
.
Rais mteule wa Marekani Donald Trump ameishutumu China kwa kuiiba meli hiyo ,huku akisema: Tunafaa kuiambia China kusalia na manuwari hiyo walioiba, aliandika katika mtandao wake Twitter..
.
Kisa hicho ni miongoni mwa visa vibaya zaidi vya makabiliano ya kijeshi kati ya mataifa hayo yenye uwezo mkubwa wa kijeshi katika kipindi cha miongo kadhaa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *