sport news

Azam yatangulia fainali Kombe la Mapinduzi

Azam FC imetinga kwenye fainali ya Kombe la Mapinduzi baada ya kuifunga Taifa Jang’ombe bao 1-0 katika mchezo wa fainali ya kwanza uliofanyika kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar.

Bao pekee katika mchezo huo, liliwekwa kimiani na Frank Domayo katika dakika ya 33 na lilidumu hadi dakika 90 za mchezo.

Kwa ushindi huo, Azam itakutana na mshindi wa mchezo wa nusu fainali ya pili utakaowakutanisha watani wa jadi Simba na Yanga utakaopigwa saa 2:15 usiku huu.

Azam ilifanikiwa kutinga nusu fainali baada ya kuifunga Yanga mabao 4-0 Jumamosi iliyopita.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *