
Kiongozi wa upinzani Rwanda, atangaza serikali mbadala
Kiongozi wa upinzani nchini Rwanda, ametangaza kuunda serikali sambamba na utawala uliopo Rwanda, lakini itakayokuwa ikifanya kazi nje ya nchi.
Thomas Nahimana ambaye ni kasisi wa zamani anayeishi nchini Ufaransa ametangaza kuunda serikali hiyo itakayofanyia kazi uhamishoni.
Katika mazungumzo na BBC, mwanasiasa huyo anasema lengo la serikali yake ni kuiondoa madarakani serikali ya rais Paul Kagame, anayemlaumu kuvunja sheria na kukandamiza wananchi.
Thomas Nahimana, amekatazwa kuingia Rwanda kujiandikisha kama mgombea wa kiti cha urais, katika uchaguzi mkuu unaopangiwa kufanyika mwezi Agosti mwaka huu.
Ametangaza tayari baraza lake la mawaziri.
Rwanda kuwapeleleza askari 20 wa Ufaransa
Rwanda yanunua ndege ya kisasa ya Airbus
Kagame: Raia wa Rwanda walitaka wenyewe
Baadhi ya aliowataja katika baraza lake la mawaziri ni wafungwa wanaotumukia vifungo vya jela nchini Rwanda kwa makosa kama vile kukanusha kuwa mauwaji ya kimbari hayakufanyika nchini Rwanda mwaka 1994.
Nahimana
Bw Nahimana, ambaye ni mhutu, amelaumiwa kwa kuandika taarifa kadhaa za kikabila na kumkosoa rais Paul Kagame.
Chama chake cha Ishema, bado hakijaandikishwa nchini Rwanda.